|
Mshambuliaji
wa Malawi, Rodrick Gonani akimtoka beki wa Eritrea, Yohannes Nega katika mchezo
wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker
Challenge, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda jioni
hii. Malawi ilishinda 3-2, mabao ya Chiukepo Msowoya dakika ya nne, Miciam Mhone
dakika ya 10 na Patrick Masanjala dakika ya 66, wakati ya Eritrea yalifungwa na
Amir Hamad Omary dakika ya 72 na Yosief Ghide kwa penalti dakika ya
89.
|
|
Kocha
wa Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ akiwa na wasaidizi wake, Mugisha Ibrahim
ambaye ni kocha wa makipa na Eric Nshimiyimana, ambaye ni Kocha Msaidizi,
wakifuatilia mchezo wa Kundi C kati ya Malawi na Eritrea Uwanja wa Mandela,
Namboole, Kampala,
Uganda.
|
|
Kocha
wa Tanzania, Kim Poulsen akiwa na Msaidizi wake, Sylvester Marsh wakifuatilia
mchezo kati ya Rwanda na Malawi. Chini ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
|
on Thursday, November 29, 2012
Post a Comment