Muwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii,Dkt. Grace Mallya akizungumza mapema jana kwenye maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam.Chimbuko la Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia ni mauaji ya kinyama ya wadada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominika mwaka 1960. Kuanzia Novemba 25 mwaka 1991, Umoja wa Mataifa uliitenga siku hii kama Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake.
Maadhimisho haya yanafikia kilele tarehe 10 Desemba ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha Tamko Rasmi la Haki za Binadamu, ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu na vile vile kutia msisitizo kwamba ukatili kama huu ni uvunjwaji wa haki za binadamu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Bi.Usu Mallya na shoto ni Muwakilishi kutoka shirika la UNFPA,Anna Holmstrom. Muwakilishi kutoka shirika la UNFPA,Anna Holmstrom nae akichangia mada mbalimbali zilizotolewa kwenye maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam jana.Chimbuko la Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia ni mauaji ya kinyama ya wadada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominika mwaka 1960.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Bi.Usu Mallya akizungumza mapema jana mchana kwenye maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam.Siku hizi 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia zimekuwa zikitumika na wadau ulimwenguni kote kama mbinu mahsusi za kutoa wito kwa jamii ili kumaliza aina zote za ukatili wa kijinsia kwa kufanya yafuatayo:-• Kujenga uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia kama uvunjwaji wa haki za binadamu kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa. • Kuimarisha kazi za kupinga ukatili wa kijinsia katika ngazi za chini na kujenga daraja kati ya kazi za maeneo mbalimbali yanayoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake. • Njia ya kubadilishana taarifa na uzoefu katika kuzuia na kupambana na ukatili dhidi ya wanawake kati ya wadau. • Njia ya kuonyesha mshikamano ulimwenguni kote kupinga ukatili wa kijinsia. • Kama chombo cha kutumia kupaza sauti ili wadau wote waweze kutekeleza wajibu wao katika kupiga vita ukatili wa kijinsia. Kila mwaka kumekuwa na kauli mbiu kuhusiana na ukatili dhidi ya wanawake. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “FUNGUKA: KEMEA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE. SOTE TUWAJIBIKE”.
Baaadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia jambo Igizo lenye mafunzo ya kupambana na kuondoa ukatili wa kjinsia likifanyika. Baadhi ya wafunzi walioshiriki maadhimisho hayo wakiimba Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia jambo kwenye maadhimisho hayo Mmoja wa wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania,Dada Lilian Liundi akifafanua jambo kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho hayo ya maadhimisho ya muendelezo wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mtando wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar Es Salaam.
Post a Comment