Afisa uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi.
Roida Andusamile (wa pili kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney
Maleko (wa pili kulia) kugawa vyeti kwa washiriki sambambamba na kufunga
Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Building
and Home Improvement EXPO 2012 Bw. Zakaria Malcom ambao ndio waandaaji wa
maonesho hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na washiriki wa
maonyesho hayo kabla ya kugawa vyeti na kisha kuyafunga rasmi ambapo amewataka
washiriki kuwasilisha Profile za makampuni yao katika mamlaka husika pamoja na
kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Saba saba yatakayofanyika
mwakani.
Pia amewataka washiriki
kujijengea utamaduni wa kuzunguka katika maduka mbalimbali yanayouza vifaa vya
ujenzi na samani za ndani kuangalia ubora wa bidhaa ili kugundua iwapo
zinachakachuliwa na wafanyabiashara wa kigeni na kuwaasa kuongeza ubora wa
bidhaa wanazozitengeneza kuwa na kiwango cha kimataifa ili kwa kushirikiana na
mamlaka yake waweze kupata soko nje ya nchi.
Meneja Masoko wa
Kampuni ya Alredha Lighting wanaopatikana Mkabala na Shoppers Plaza Mikocheni
Bw. Riyaz Jetha akipokea cheti cha ushiriki bora katika maonyesho hayo kutoka
kwa Bi. Jacqueline Mneney Maleko.
Pichani Juu na Chini
baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani
wakipokea vyeti vyao vya ushiriki bora.
Mwakilishi wa Kampuni
ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter akipokea
cheti.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akibadilishana mawazo na baadhi
ya washiriki wa maoneysho hayo. Kulia ni Meneja Mauzo Afrika Mashariki wa
Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa na Katikati ni Mwakilishi wa
Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara
Peter.
Meneja Mauzo Afrika
Mashariki wa Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa akionyesha uimara
wa moja ya bidhaa zinazopatikana katika duka la Alredha
Lighting.
Pichani Juu na Chini ni
baadhi ya washiriki wa Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za Ndani
yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na
kufungwa jana. Maonyesho hayo yaliyodumu kwa siku tatu yaliandaliwa na Kampuni
ya Tanzania Building and Home Improvement EXPO
2012.
Post a Comment