* AAMUA KUWATWISHA ZIGO LILILOMSHINDA KWA SADC
MGOGORO wa
kugombea nani ni mmiliki wa Ziwa Nyasa kati ya nchi za Tanzania na Malawi
umezidi kuwa mgumu baada ya kushindwa kuafikiana tena leo kati ya kikao cha
mawaziri wa nchi hizo mbili pamoja na wanasheria wao.
Kutokufikia mwafaka huku kumejitokeza leo baada ya kikao hicho hivyo pande zote kukubaliana suala hilo liende kuamuliwa na jopo la marais wastaafu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Hata hivyo Tanzania imesema endapo SADC watashindwa kutatua suala hilo litapelekwa tena katika Mahakama ya Usuluishi wa Migogoro Kimataifa ili haki ipatikane.

Mvutano huo umeibuka
zaidi pale nchi ya Malawi ilipoanza kuingiza makampuni ya utafiti wa mafuta na
gesi ambayo yaliingia na kuweka kambi hadi maeneo ya Tanzania. Tanzania imekuwa
ikiamini ziwa hilo ni miliki ya nchi hizi mbili, huku Malawi ikipinga na kutaka
itwae ziwa lote.
Post a Comment