Baadhi ya wahariri wa
vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika
mkutano huo
Prof. Meena (kulia)
akifafanua jambo..
Mmoja wa wahariri kutoka
vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jane Mihanji na
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)
akichangia mada katika mkutano
*****************
Na : Mwandishi wa
Thehabari.com
KAIMU Mkurugenzi wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mary Nsemwa amevipongeza vyombo mbalimbali
vya habari nchini kwa kile sasa kutoa nafasi ya kuridhisha kwa kuandika masuala
mbalimbali ya kijinsia ambayo hapo awali yalikuwa hayapewi nafasi ya
kutosha.
Bi. Nsemwa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari katika mkutano wao na TGNP, kuzungumzia changamoto anuai za kijinsia na vyombo vya habari pamoja na ushiriki wa wanawake katika mchakato wa maoni ya uundwaji wa katiba mpya.
Alisema ushirikiano mzuri uliojengeka kati ya taasisi hiyo na vyombo vya habari umesaidia kwa kiasi kikubwa hivyo masuala ya kijinsia na hasa yale yanaowakandamiza wanawake kusikika katika vyombo vya habari hali ambayo imesaidia kwa kiasi fulani.
“…Tumejifunza mengi kutoka katika vyombo vya habari, vyombo hivi sasa vimewaunganisha wanawake…sauti za wasiosikisa hasa wa vijijini sasa zinasikika kupitia vyombo hivi. Vyombo vya habari pia vimepaza sauti kwa kampeni yetu ya Haki ya Uchumi; ‘Rasilimali Ziwanufaishe Wanawake walioko Pembezoni’ na mkumbuke kwamba nyinyi mnanguvu zaidi yetu,” alisema Bi. Nsemwa.
Naye mmoja wa Wajumbe wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Profesa Ruth Meena
akiwasilisha mada katika mkutano huo wa wahariri alisema mambo mengi ya msingi
ambayo ni miongoni mwa madai ya wananchi yameainishwa katika Katiba iliyopo
sasa, hivyo kushauri ipo haja ya kuangalia namna ya usimamizi wa sheria na
mabadiliko kadhaa kuingizwa kwenye Katiba Mpya.
“...Kwa upande
mmoja Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa haki sawa
kwa wanawake na wanaume katika nyanja za siasa, uchumi na ustawi wa jamii, na
hapohapo kuzipokonya kwa mkono mwingine kwa kuruhusu kuendelezwa kwa sheria,
taratibu na tabia zinazokinzana na katiba,” alisema Prof.
Meena.
Aidha alishauri Katiba
mpya ibatilishe sheria zote zinazokinzana na haki za msingi za wanawake na
watoto wa kike hususani kubatilisha sheria na mila zote za ubaguzi wa jinsia,
ubaguzi dhidi ya watoto hususani watoto wa kike, katika maswala ya ndoa,
mirathi, haki za kumiliki.
“Kwa
mantiki hii, katiba ibainishe kwa uwazi haki za wanawake na haki za watoto.
Pamoja na kuwajibisha serikali kuchukua hatua zote za kisera na sheria ili
kulinda na kuhifadhi haki za wanawake na za watoto katika maeneo hayo, na
pia iwajibishe serikali kutekeleza mikataba yote iliyoridhia
kuhusu haki za wanawake ( CEDAW, CRC, ILO Conventon) Mikataba hii itambulike
kuwa ni sheria za nchi ili kuepusha ucheleweshaji wa kutafsri au kuruhusu
uchakachuaji wamikataba hii katika sheria za nchi,” alifafanua Prof.
Meena.
Pamoja na
hayo alishauri Katiba mpya iangalie haki ya ufikiaji wa huduma za jamii;
haki ya kufikia na kufaidi huduma za msingi kama vile maji,
chakula, malazi na elimu na hifadhi ya jamii ziendelee kuwepo - pamoja na
kusisitiza wajibu wa serikali wa kuhakikisha huduma hizi za msingi
zifikiwe na ke na me ( rika zote, na hali zote).
-Habari hii imeandaliwa na
Mtandao wa www.thehabari.com
Post a Comment