Alex
Mgongolwa, Mwenyekiti wa kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji ya
TFF
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
17
Novemba 2012
Katika kikao chake cha
tarehe 3 Novemba 2012, Kamati ya Utendaji ya TFF ilipokea taarifa ya mapendekezo
ya marekebisho ya Katiba TFF kama ifuatavyo:
Kuingiza kipengele
kinachohusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa
na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF, ikiwemo TFF,
kuhakikisha kuwa kipengele hicho kinaingizwa katika katiba
zao.
Kutokana na ushauri na
maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchanguzi
(“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao hivi sasa
ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa
ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
Kuindoa nafasi ya Makamu
wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika
Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe. Hii inatokana
na azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha
kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni
zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na
kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
Baada ya kutafakari
mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF iliamua
kuwa:
Ipo haja ya kuifanyia
marekebisho Katiba ya TFF kama iliyopendekezwa.
Kwa vile mapendekezo
mawili kati ya matatu ya ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu
wa TFF, ipo haja ya marekebisho hayo kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano
Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa
TFF.
Aidha, kwa vile TFF
haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya
marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi
kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular
Resolution”).
Waraka huo (“Circular
Resolution”) uwe umeshatayarishwa na Sekretariati ikishirikiana na Mwenyekiti wa
Kamati ya Sheria ifikapo tarehe 15 Novemba 2012 na ukabidhiwe kwa Wajumbe wa
Kamati ya Utendaji wanaowakilisha Kanda za TFF ambao watahakikisha kuwa kila
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Kanda husika anapata fursa ya kutoa ridhaa
yake.
Zoezi la kupata ridhaa
ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu liwe limemalizika katika kipindi cha siku
21.
Kikao kinachofuata cha
Kamati ya Utendaji kitafanyika Jumamosi tarehe 15 Desemba 2012 kwa madhumuni ya
kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano Mkuu. Katiba ya
TFF inaelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa wanachama wake angalau
siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano. Hivyo Kamati ya utendaji inatarajia
kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 16 na 17
na Februari 2013.
Kamati ya Utendaji ya
TFF inasisitiza kuwa utaratibu huu umeamuliwa kutokana na TFF kutokuwa na uwezo
wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika kipindi kifupi kijacho.
Kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano Mkuu, jambo ambalo hatuna
budi kuliepuka.
Kamati ya Utendaji ya
TFF inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa jumla ili kufanikisha zoezi hili na
hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa
TFF.
Wenu Katika
michezo,
Alex
Mgongolwa
Mwenyekiti
KAMATI YA SHERIA,
MAADILI NA HADHI ZA WACHEZAJI
Post a Comment