
Simone Gbagbo
Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa
kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi
Simone, Gbagbo.
Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na
uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya
uchaguzi wa urais nchini humo.
Mumewe tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake
kuanza katika mahakama hiyo iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya
uhalifu wa kivita.
Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko
yaliyotokea baada ya ya Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa
Urais.
Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki
moja Aprili mwaka wa 2011, miezi mitano, baada ya uchaguzi wa
urais.
Wanajeshi wa rais wa sasa wakiungwa mkono na
wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walianzisha msako mkali dhidi yao, baada ya
kujificha ndani ya ikulu ya rais.
anatuhumiwa kuhusika na mauaji, ubakaji, dhuluma
na ngona na kuwadhulumu wapinzani wa serikali miongoni mwa mashtaka mengine
mjini Abidjan.
Licha ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti
chochote cha kisiasa, ripoti zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa
alimshawishi mumeo kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo, 67, alihamishwa hadi The Haque mwaka
uliopita, na kuandikisha historia ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa
mbele ya mahakama hiyo ya ICC.
Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo
yote.
Kabla ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na
mkewe mwenye umri wa miaka 63, walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast
kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi, ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na
kutumia rasilimali za umma kwa njia mbaya
Mahakama hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa
serikali ya Ivory Coast, kumusafirisha Bi Gbagbo ili afunguliwa mashtaka huko
the Haque.


Post a Comment