Na Mwandishi wa
EANA
Waziri wa Biashara wa
Sweden, Ewa Bjorling amewapa changamoto wafanyabiashara na wanawake nchini mwake
kutumia nafasi nyingi zilizopo kuwekeza katika kanda ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC).
Akihutubia umati mkubwa
mjini Stockholm, Sweden hivi karibuni,kwenye Jukwaaa la Kwanza la Wanyabiashara
wa Sweden na EAC, Waziri huyo alisema kwamba uwekezaji unakua kwa haraka katika
kanda hiyo na kusisitiza kwamba kanda hiyo ina mazingira bora ya kuweza kufanya
biashara.
‘’Kanda ina nafasi lukuki
katika sekta za madini, utengenezaji bidhaa, afya, kilimo na huduma za teknolojia ya habari na
mawasiliano (ICT),miongoni mwa nafasi zilizopo,’’ aliuambia mkutano huo na
kuongeza kwamba Afrika hivi sasa inakuja juu kwa maswala ya uwekezaji na
imejipanga kuwa katika hali nzuri zaidi kiuchumi siku za usoni.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Sekretarieti ya EAC na nakala yake kupatikana kwa Shirika Huru la
Habari la Afrika Mashariki (EANA), Waziri Bjorling alieleza kwamba EAC
imeonyesha uwezo wa kufanya mabadiliko, kukuza uchumi na kuleta
maendeleo.
Naye Katibu Mkuu wa EAC,
Dk. Richard Sezibera kwa upande wake alisema kwamba, wakati kanda ya EAC
inatafuta wawekeaji, wafanyabiashara wa kanda hiyo pia hawana budi kusaka nasafu
zinazopatikana nchini Sweden.
‘’Raia wa EAC nao
wanahitaji kuzisaka nafasi za kuwekeza zinazotolewa na Sweden.Ninaamini kwamba
hatua hiyo itatoa nafasi muafaka baina ya pande zote mbili kuimarisha uchumi,’’
alisisitiza.
Katibu Mkuu pia
alikaribisha majadiliano baina ya Chama cha Wafanyabishara cha Sweden na Chama
cha Wanawake Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kwa lengo la kuhamasisha ujuzi
kwa wanawake ili kuunganisha nafasi za biashara baina ya pande hizo
mbili.
Mapema Kiongozi wa Mabalozi
wa EAC nchini Sweden kutoka nchini Uganda, Joseph Tomusange alisema kuwa EAC ni
eneo lenye amani na ni salama kwa uwekezaji.
Mkutano huo pia
ulihudhuriwa na wawakilishi wa mawakala wa uwekezaji kutoka nchi wananchama wa
EAC ambao walitoa maelezo juu ya nafasi za uwkezaji zilizopo na manufaa
yake.



Post a Comment