Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Ndugu Zenno
Ngowi aliseme ‘’Upatikani wa makazi ya uhakika na upatikanaji wa masuluhisho ya
ujenzi wa nyumba bado umeendelea kuwa changamoto kubwa kwa Watanzania wengi.
Hata hivyo, katika kipindi hiki Nchini Tanzania tumeshuhudia kukua kwa kasi kwa
sekta ya nyumba na huduma nyingine za ujenzi katika siku za karibuni. Hata hivyo
uwepo wa taarifa sahihi juu ya masuluhisho mbalimbali yahusuyo sekta ya nyumba
limekuwa nin tatizo kubwa, upungufu huu ndio ulikuwa msingi Mkuu wa kuanzisha
maonyesho ya Tanzania Homes Expo’’
Zenno aliongeza kusema ‘’Ni
jambo la kujipongeza kuona mabenki kadhaa yanatoa mikopo ya nyumba, lakini
taarifa za kina namna ya kupata mikopo hii raia wengi hawajui!, Je ni mara ngapi
imebidi mtu kusimamia nyumba yake mwenyewe wakati wataalam na macontractor wapo!
Je kabla ya kuchagua aina ya nyumba ya kujenga tunajua mambo muhimu ya
kuzingatia? Jibu ni hapana’’.
Tanzania Homes Expo, ni
maonyesho yenye lengo la kukuza elimu ya umma kuhusu aina mbali mbali za huduma
zinazolenga sekta hii muhimu. Lakini pia Tanzania Homes Expo inatoa fursa kwa
watoa huduma za sekta ya nyumba kama; mabenki, mikopo, bima, wakandarasi,
wachora ramani, makampuni ya nyumba, makampuni ya ulinzi, marembo, vifaa vya
ujenzi na mengi yahusuyo sekta ya nyumba kupata nafasi ya kuelezea huduma
wanazozitoa.
Tanzania Homes Expo
inadhaminiwa na Azania Bank, Clouds FM, TMRC na Brand
Works.
Kwa taarifa zaidi au
kushiriki tembelea tovuti; www.tanzaniahomesexpo.org au tuma barua pepeinfo@tanzaniahomesexpo.org




Post a Comment