KATIBU Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana amewahakikishia Watanzania, hususan wanachama wana-CCM kwamba
yupo tayari kimwili na kiakili kuhakikisha anatekeleza kwa ufanisi mkubwa
majukumun makubwa aliyopewa kulitumikia taifa.
Kinana alisema hayo leo
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Rukwa akiwa katika siku yake ya pili
ya ziara ya siku nne katika mikoa ya Mtwara, Rukwa, Geita na Arusha aliyoianza
jana.
“Ni kweli nilikuwa
nimetangaza kustaafu siasa kwa kuzingatia kwamaba nimeshashika kwa muda mrefu
nyadhifa za kuchaguliwa, nikaona kwamba kama wenzako wameshakuamini mwa muda
mrefu ukafanya nao kazi wakikupenda, basi usisubiri mapaka uchokwe ndiyo
uondoke”, alisema Kinana na kuongeza;
“Lakini sasa baada ya
maamuzi yangu, Mwenyekiti wa Chama Chetu, Rais Jakaya Kikwete akaamua kwa kadiri
alivyoona inafaa, akaniteua nikisaidie Chama. Kwa mtu mwenye hekima na uadilifu
unapoteuliwa na Mwenyekiti wa Chama chako tena Rais wa Chama kinachotawala,
lazima ukubali tena bila kinyongo, nikakubali”.
“Sasa baada ya kuwa mimi
ndiye Katibu Mkuu wa Chama hiki, napenda kuwaambia kwa dhadi ya moyo wangu
kwamba nipo tayari, kimwili, kiakili kuhakikisha nawatumikia Wana-CCM na
watanzania kwa jumla kwa weledi na ufanisi
mkubwa”.



Post a Comment