Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Sheikh Amr Abeid, baada ya kuvalishwa mavazi ya heshima ya moja ya makabila ya mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Aggrey Mwanri akihutubia kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Baadhi ya wananchi wakipigapicha kwa kutumia kamera na simu zao ili kupata kumbukumbu ya matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Khamis Sadifa Juma. akizungumza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Aliyekuwa diwani wa Chadema, Rehema Mohammed ambaye amehamia CCM, akibubujikwa machozi jukwaani wakati akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wakijikinga mvua kwa mkeka wakati wa mkutano huo.
Maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza ‘kiduku’ Msanii Marlow alipotumbuiza wakati wa mkutano huo.