WATU wawili wanaoishi mtaa mmoja na Marehemu Sharo Milionea, wamefariki dunia usiku huo huo aliofariki Sharo Milionea.
Nyumba mbili zinazofuata na nyumba aliyopanga Sharo Milionea walifariki na kufanya nyumba zote tatu zinazofuatana ziwe msibani.
Sharo Milionea aliyezikwa jana nyumbani kwao Lusanga, Muheza Mkoani Tanga, alipanga nyumba maeneo ya Sinza B jirani na Palestina, nyumba ambayo haina zaidi ya wiki moja tangu ahamie na kulipia kodi ya mwaka mzima.
Kufuatia misiba hiyo mingine miwili iliyowahusisha wanawake wawili, baadhi ya watu walizingirwa na utata mwingi na kuona kama ni matukio ambayo si ya kawaida na wako hata walithubutu kusema mtaa huo una ‘gundu’.
Mama mwenye nyumba wa Sharo Milionea anasema siku ya tukio alimpigia simu Sharo na kumwambia asisahau kuja kuwasha taa ya nje, kwa mujibu wa mama huyo, Sharo alifika kati ya saa 11 na saa 12 jioni kuwasha taa na ndipo safari yake ya kwenda Tanga ikaanza.
Chanzo cha tovuti ya Saluti5.com kimesema majirani hao wa Sharo Milionea wote wanatarajiwa kuzikwa leo.
Post a Comment