RAIS wa klabu ya AC Milan ya Italia, Silvio
Berluscon
MILAN, Italia
Baada ya kufika alimkumbatia yoso Stephan El Shaarawy,
ambaye alilitoa bao lake la kwanza la kimataifa dhidi ya Ufaransa Jumatano kwa
Berlusconi, kisha kupeana mikono na wachezaji wote na kocha wao Massimiliano
Allegri
RAIS wa klabu ya AC Milan ya Italia, Silvio Berlusconi
alilazimika kusafiri kwa helikopta janai Ijumaa kwenda kwenye mazoezi ya timu
yake kuamsha hamasa kuelekea pambano lao la Serie A leo Jumamosi dhidi ya
Napoli.
Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Italia ambaye aliwasili
Milanello kwa helikopta na kutembelea uwanja wa mazoezi, alizungumza na
wachezaji wa kikosi hicho kwa dakiika 10, Gazzetta dello Sport limeripoti tukio
hilo.
Baada ya kufika alimkumbatia yoso Stephan El Shaarawy,
ambaye alilitoa bao lake la kwanza la kimataifa dhidi ya Ufaransa Jumatano kwa
Berlusconi, kisha kupeana mikono na wachezaji wote na kocha wao Massimiliano
Allegri.
Berlusconi akaiambia Milan Channel kuwa: "Kama Allegri yuko
hapa, basi ni kwa sababu yeye yuko katika imani yangu."
Ziara ya ghafla ya Berlusconi ililenga kuichagiza Milan,
iliyo katika hali ngumu msimu wa Serie A inakoshika nafasi ya 13 ikiwa na pointi
14.
Kikosi hicho kimepoteza jumla ya mechi sita kati ya 12,
ambapo kabla ya leo kuivaa Napoli, wiki iliyopita ilikubali kichapo cha mabao
3-1 nyumbani San Siro kutoka kwa Fiorentina.
Katika mechi ya leo, Milan ilitarajia kumkosa beki wake
Daniele Bonera ambaye atakuwa nje ya dimba kwa wiki tatu, baada ya kuumia mguu
wa kushoto katika kichapo cha Fiorentina.
Post a Comment