LONDON, England
'Alikuwa na miaka 16. Nikamuuliza kama yuko tayari
kufanya majaribio na kikosi cha wakubwa, akakataa. Je napaswa kujuta katika
hilo? Hapana. Kama mtu anakwambia ana ubora unaouhitaji, bila shaka unapaswa
kujiridhisha, vinginevyo haiwezekani'
SAA 24 baada ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kufanya
kufuru dimbani, Mfaransa anayeinoa Arsenal, Arsene Wenger amesema hajutii
kumpoteza mkali huyo wakati alipoenda klabuni Highbury kufanya majaribio akiwa
na miaka 16.
Nyota huyo wa klabu ya Paris St German kwa sasa, amepamba
vichwa vya habari wiki hii, kutokana na mabao yake yaliyoipa Sweden ushindi wa
4-2 dhidi ya Engalnd, likiwamo moja zuri zaidi kuwahi kufungwa.
Mabao hayo yamefuatiwa na tambo mbalimbalimbali kutoka kwa
Ibrahimovic, wengi wakirudi nyuma na kukumbuka kauli yam kali huyo aliyomwambia
Wenger wakati alipotua klabuni Highbury mwaka 2000 kuwa 'Yeye sio wa kufanyiwa
majaribio.'
Yoso mwingine Cristiano Ronaldo ni kati ya wakali walioonwa
na macho ya Wenger, sanjari na mkali wa sasa wa Man City, Yaya Toure aliyekuwa
akisakata soka nchini Ubelgiji wakati huo.
Ndipo Ibrahimovic alipojiunga na Ajax, kabla ya kushinda
mataji akiwa na AC Milan, Barcelona na Inter, huku akiweka rekodi ya dau la
jumla la uhamisho wake kufikia pauni milioni 150. Pia akikumbukwa kwa kuichapa
Arsenal mabao matatu na kuing’oa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Na sasa Wenger anafungua kinywa kusema: 'Alikuwa hapa kwa
majaribio na kisha amkaenda zake sehemu nyingine. Hilo limetokea kwa wachezaji
wengine: Ronaldo, Ibrahimovic. Habari hiyo ni kweli kwamba nilihitaji kumuona,
lakini sikuwa namfahamu.
'Alikuwa na umri wa miaka 16. Nikamuuliza kama yuko tayari
kufanya majaribio kidogo na kikosi cha wakubwa, akakataa kufanya hivyo.
'Je napaswa kujuta katika hilo? Hapana. Kama mtu anakwambia
kuwa yeye ana ubora unaouhitaji, bila shaka unapaswa kujiridhisha binafsi kwa
kumuangalia, vinginevyo haiwezekani.'
Nyota ya Ibrahimovic kwa sasa ni angavu mno, kutokana na
alichofanya katika ushindi huo wa mechi ya kirafiki, zaidi likiwa ni bao lake la
mwisho katika dakika ya 90+1 alilopiga ‘tik-tak’ akiwa umbali wa mita 30 na
kufunga
Post a Comment