MADRID, Hispania
“Yeye ni mtu wa ajabu sana. Binadamu muungwana.
Alinifundisha mambo mengi sana.
Kama nilivyowahi kusema hapo kabla kuwa, yeye kwangu
mimi ni kama baba katika soka”
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo (pichani juu), amedai kuwa
kama mchezaji, bado anajihisi kumpoteza na kukosa vitu muhimu vya Sir Alex
Ferguson kama kocha wake.
Nyota huyo wa klabu ya Real Madrid mwenye umri wa miaka 27,
alitumia jumla ya misimu sita akiwa chini ya Fergie klabuni Old Trafford, kabla
ya kuhama na kutimkia Bernabeu – na bado atakuwa mbali na kocha wake wa zamani
kwa miaka mitatu ijayo.
Ronaldo alisema: “Yeye ni mtu wa ajabu sana. Binadamu
muungwana. Alinifundisha mambo mengi sana.
“Kama nilivyowahi kusema hapo kabla kuwa, yeye kwangu mimi
ni kama baba katika soka. Kimsingi nimepotezana naye na kumkosa na mahusinao
yangu kwake kwa ujumla.”
Licha ya kumkumbuka, lakini Ronaldo alifichua kuwa, Fergie
angali imara na mkali kwa wachezaji wake, licha ya ukweli kuwa anatarajia
kutimiza umri wa mika 71 hapo Desemba.
Ronaldo akaongeza kuwa: “Fergie bado imara. Nadhani yeye
hawezi kuwa hivyo kwa sababu, upi umri wake? Miaka 70? Sio mzuri kwa moyo
wake.
“Yeye bado imara, mwenye nguvu, nakumbuka mara yangu ya
kwanza kabisa, nilimuona akiwa na nguvu sawa na alizonazo sasa,” alikumbuka
Ronaldo.
Post a Comment