RAIS
Jakaya Kikwete amesema serikali ina mpango wa kujenga uwanja wa ndege wa
kimataifa katika mji wa Mugumu, wilayani Serengeti, ili kurahisisha usafiri kwa
watalii waendao au kutoka kwenye vivutio vya utalii vilivyopo kanda ya
kaskazini.
Amesema
hayo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM unaoendelea mjini
Dodoma.
Kauli
hiyo ya mwenyekiti wa ccm ameitoa alipokuwa akifafanua kuhusu taarifa iliyosomwa
na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, mbele ya wajumbe hao kuwa
serikali itajenga kiwanja hicho.
Akitoa
ufafanuzi huo, Rais Kikwete amewaeleza wajumbe hao kwamba uwanja utakaojengwa
utakuwa eneo la Mugumu na sio kwenye Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Amesema
kuwa hatua hiyo ya ujenzi wa kiwanja hicho cha ndege utawawezesha watalii
uchaguzi wa ama kutua Mugumu au Uwanja wa Kimataifa wa
Kilimanjaro.
Amesema
kwa watalii watakaoshukia uwanja wa KIA na kutembelea hifadhi ya Tarangire,
Manyara, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wataweza kuondoka kurejea
makwao kwa kutumia uwanja utakaojengwa Mugumu badala ya kurudi tena hadi
KIA.
Hali
kadhalika amesema, watalii watakaoshuka kwenye uwanja utakaojengwa Mugumu
hawatakuwa nahaja ya kurudi tena Serengeti ili warejee makwao kwa kuwa
wataendelea kutembelea vivutio vingine kwenye katika Hifadhi za Manyara,
Tarangire, Anapa hadi Mlima wa Kilimanjaro na kurejea makwao kwa kutumia uwanja
wa KIA.
Akizungumzia
kuhusu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, dk kikwete amesema
umekwishakamilika na uzinduzi wake unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka
huu.
Amesema
uwanja huo uko kusini na yapo mashirika kadhaa ya ndege ya kimataifa ambayo
yameomba ndege zao ziwe zinatua kwenye uwanja huo wakati zikifanya safari zake
za kwenda nchi za Kusini mwa Afrika.
Aidha
amesema upo mpango kabambe wa kulitumia eneo la ukanda wa Nyanda za Juu Kusini
kwa kilimo kikubwa cha maua ambayo yatakuwa yakisafirishwa kwenda kuuzwa nje
kupitia uwanja huo.
Ametanabaisha
kuwa kwa sasa serikali itaelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kanda ya Nyanda
za Juu Kusini, inapewa msukumo kwa kilimo kikubwa cha maua ambacho tutakipa
nguvu zaidi ili yasafirishwe kwenda kwenye masoko ya
nje.
RAIS Jakaya
Kikwete amesema baada ya kupatikana kwa gesi asilia kiasi cha mita za ujazo
trilioni 33 , serikali kwa kuanzia inatarajia kujenga gridi ya taifa ya gesi
jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya matumizi ya viwandani na
majumbani.
Amesema
gesi itakayopatikana itatumika kwa matumizi ya viwandani na majumbani na kiasi
kingine kitauzwa nje.
Amesema
baada ya kukamilika giridi ya gesi, wakazi wa Dar es Salaam watakaohitaji kupata
gesi hiyo kwa matumizi ya majumbani kwao watapelekewa.amesema utaratibu kama huo
utafanyika kwa mikoa mingine.
Amesema
upatikanaji wa gesi hiyo utaifanya Tanzania iweze kukuza uchumi wake kwa kuwa
itatumika kwa uzalishaji wa bidhaa viwandani, mbolea na uzalishaji wa
umeme.
Hata
hivyo, amesema gesi itayouzwa nje itasafirishwa kwa kupitia bandari za Mtwara na
Kilwa kwa kuwa itakuwa gharama kuisafirisha hadi Dar es Salaam katika lengo la
kuiuza nje.
Amesema
sera ya gesi inatarajiwa kukamilika hivi karibuni pamoja na kuweka miundombinu
itakayowezesha kudhibiti uhujumu wa biashara hiyo nje ya
nchi.
Post a Comment