Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na
Jacqueline Namfua, Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia
Watoto Duniani (Unicef) wakati wa semina ya waandishi wa habari.
Namfua alisema kuwa vifo vya watoto wachanga chini
ya miaka mitano vimepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema hali hiyo inatokana na wananchi wengi kuelimishwa na kufuatilia huduma
za chanjo mara kwa mara.
Aliwataka wananchi washilikiane katika kuhakikisha
kila mwenye mtoto anapelekwa kupata chanjo ili kuepuka magonjwa kama surua,
pepopunda na polio ambayo yana wanyemelea watoto wenye umri mdogo kuanzia mwaka
mmoja nakuendelea.
Hata hivyo, alisema bado kuna changamoto kubwa
kuhakikisha vifo vya watoto venye umri mdogo vinapungua hadi kufikia asilimia
100.
Alitoa wito kwa wananchi kuwapeleka watoto katika
vituo vya kupata chanjo.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment