Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wakuu
wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mjini Dodoma
juzi.
Mkurugenzi wa Masoko na
Utafiti, Raphael Mwamoto akitoa mada ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa na
Wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mwantumu Mahiza akichangia jambo katika kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Joseph Simbakalia akitoa mchango wake.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,
Stella Manyanya akichangia mada katika kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi
hicho wakifuatilia mada ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
SERIKALI imeshauriwa
kubadili utaratibu wa matibabu kwa Maofisa Waandamizi ili kuwawezesha kunufaika
na huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Ushauri huo umetolewa na
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mjini Dodoma katika kikao kazi cha siku tatu
ambacho kiliongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Wamesema kuwa utaratibu
wa sasa ambao unaonesha kuwa matibabu ni moja ya stahiki zao unawazuia Wakuu hao
kunufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF ambazo walisema zimeboreshwa sana
kwa sasa na zina mtandao mkubwa unaowezesha kupata huduma mahali popote
nchini.
Akichangia mada
iliyowasilishwa na NHIF kwa wakuu hao, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a
alisema kuwa “Tunataka kuwa wanachama wa NHIF hata sasa ila kinachotubana ni
hizo stahiki ambazo tumepewa ikiwemo ya matibabu kulipiwa na Serikali, ipo haja
sasa ya Serikali kupeleka fedha NHIF ili sisi tutibiwe na Mfuko,” alisema
Chang’a.
Alisema kuwa ni vyema
wakajiunga na NHIF ambayo itawasaidia kunufaika na fao la wastaafu lakini pia
itawapa hamasa kubwa katika uhamaishaji kutokana na ukweli kwamba watakuwa
miongoni mwa watumiaji wa huduma hizo.
Akijibu hoja hiyo,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa kwa sasa wakuu hao wanaweza wakajiunga
wakati Serikali ikiliangalia suala hilo ili liwe kwenye utaratibu
wanaoutaka.
Akitoa maelezo ya awali
kwa viongozi hao, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba alisema kuwa ili Mfuko
ufanikiwe kuwafikia Watanzania wengi kama nchi zingine zilizofanikiwa katika
suala hilo ni lazima viongozi wakawa wanachama au wanufaika wa huduma za
Mfuko.
“Nchi zilizofanikiwa
kuwaingiza wananchi wake kwenye utaraibu wa Bima ya Afya kama Ufilipino, Korea,
Rwanda viongozi wake Wakuu ni wanachama wa Mifuko hiyo… hivyo nanyi wakuu wetu
mkijiunga itakuwa ni kazi rahisi kufikia malengo yetu,” alisema
Humba.
Aidha aliwaomba wakuu
hao kuhakikisha wanafuatilia fedha zinazolipwa na NHIF katika Vituo vya Kutolea
huduma kwenye maeneo yao ili zisaidie kuboresha huduma za matibabu ikiwemo
ununuzi wa dawa na Vifaa tiba.
Katika suala hilo la
Malipo, Waziri Mkuu aliutaka Mfuko kuweka utaratibu wa kuwapa taarifa za fedha
viongozi wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wilaya, wabunge ili waweze kuzifuatilia katika
matumizi yake.

Post a Comment