Viongozi wa nchi za
Afrika Magharibi wamekubali kupeleka kikosi cha wanajeshi 3,300 nchini Mali
kuweza kutwa udhibiti wa eneo la Kaskazini kutoka kwa wapiganaji wa
kiisilamu.
Kwenye mkutano wa nchi
wanachama wa shirika la Ecowas, mwenyekiti wa shirika hilo, alisema liko tayari
kutumia nguivu kupambana na makundi ya kigaidi pamoja na mitandao ya
uhalifu.
Makundi ya kiisilamu na
waasi wa Tuareg walichukua udhibiti wa eneo la Kaskazini mwa Mali baada ya
aliyekuwa Rais Kupinduliwa mwezi Machi.Wanajeshi watatolewa na Nigeria,Niger na
Burkina Faso.
Rais wa Ivory Coast
Alassane Outtara aliambia waandishi wa habari nchini Nigeria kuwa wanajeshi
wataanza kazi pindi Umoja wa Mataifa utakapoidhinisha mkakati huo wa
kijeshi.
Aliongeza kuwa anatumai
baraza la usalama litaidhinisha mpango huo mwishoni mwa Novemba na
Disemba
Kulingana duru za jeshi
la Mali, mpango huo utachukua kipindi cha miezi sita huku kukiwa na maandalizi
mwanzo kabla ya mafunzo kwa wanajeshi hao, pamoja na kuandaa kambi zao na kisha
baadaye jeshi kuanza harakati zake Kaskazini mwa nchi.
Umoja huo ulikuwa umetoa
muda wa siku arobaini na tano kwa viongozi wa Afrika kuanzia tarehe 12 mwezi
Oktoba kuunda mkakati wa kijeshi kuweza kuingilia kati mzozo unaoendelea
Kaskazini mwa nchi.
Post a Comment