Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Warioba: Katiba itapatikana kwa wakati



MWENYEKITI wa Tume ya kukusanya maoni kwa ajili ya Katiba mpya, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amewahakikishia Watanzania kwamba Katiba mpya itapatikana kwa wakati.
Jaji Warioba alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akijibu tamko la Jukwaa la Katiba Tanzania (Juwata) lililodai kwamba ni ndoto kuipata Katiba mpya mwaka 2014 badala yake kuitaka tume hiyo kuwaeleza ukweli Watanzania.
Katika maelezo yake Jaji Warioba alisema tume hiyo ina wajumbe 30 watakaofanya kazi kwa miezi 18 na kuhakikisha Tanzania inapata Katiba mpya ifikapo Aprili 26, 2014.
“Tulipopewa jukumu hili tulichukua muda mrefu kujipanga tangu Mei hadi Julai tukijua lazima twende sawa na muda… mpaka sasa tumeonana na watu 900,000 sio lazima kuwafikia Watanzania wote kwa sababu hii sio kura ya maoni.
Tunachofanya tunapata mawazo ya wachache kwa niaba ya wengine halafu tunapiga kura ya maoni hapo sasa ndiyo tunawahamasisha wote wajitokeze,” alisema.
Alifafanua kuwa kazi yao itaisha Oktoba 2013 na kuacha jukumu hilo kwa Bunge la Katiba, hivyo akahoji kuwa huyo anayesema hawawezi kwenda na muda anayatoa wapi maneno hayo?
Kuhusu muda wa kufanya mikutano, Jaji Warioba alimtaka mwenyekiti wa Jukata, kueleza ni muda sahihi wa kufanya mikutano na kuuliza pengine mtoa madai anataka wafanye mikutano usiku?
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za tume hiyo kwa mizunguko mitatu ya awamu ya kwanza, mwenyekiti huyo, alisema wamefanya mikutano 522 kwenye mikoa tisa.
“Awamu ya tatu iliyoishia Novemba 6, mwaka huu, tulipanga kufanya mikutano 496 ya hadhara tukafanya mikutano 522, awamu ya pili tume ilifanya mikutano 449 wakati ile ya kwanza tulifanya mikutano 388.
“Katika awamu ya tatu jumla ya wananchi 392,385 walihudhuria mikutano yetu, 21,512 walitoa maoni yao kwa kuzungumza na wengine 84,939 walituandikia,” alisema.
Aidha alibainisha kwamba idadi ya wachangiaji kwa njia ya maandishi, ujumbe mfupi wa simu za mkononi, mtandao wa kijamii wa facebook, barua pepe na barua za kawaida imeongezeka.
Chini ya uenyekiti wa Jaji Warioba wajumbe wengine ni aliyekua Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhan, ambaye ni Makamu mwenyekiti wa tume hiyo.
Jana, tume hiyo ilianza awamu ya nne ya mzunguko wa kwanza kwa mikoa ya Dar es Salaam, Simiyu, Arusha, Geita, Mara na Mjini Magharibi ili kukamilisha mzunguko wa mikoa yote ya Tanzania.

chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top