Wanavijiji nchini Kenya kaskazini wanahofia kuzuka kwa mapigano zaidi baada ya takriban polisi 29 kuuwawa mwishoni mwa wiki.
Polisi hao walivamiwa
walipokuwa wanajaribu kurudisha ng'ombe waliokuwa wameibwa.
"Tunahofia kwamba
maafisa wa ulinzi waliojawa na hasira huenda wakawashambulia wananchi wasio na
hatia kwani waliowaua polisi hao wameshatoroka," alidokeza kiongozi huyo."Hali
ni ya wasiwasi sana, huku walinda usalama waliojihami kwa silaha wakipiga doria
vijijini," kiongozi mmoja wa kidini huko Kaunti ya Samburu
alisema.
Aidha alisema kwamba
kungali kuna miili mingine ambayo haijapatikana.
Wasamburu na Waturkana
huibiana mifugo mara kwa mara. Pia hupigania maeneo ya lishe kwa mifugo na
maji.
Kulingana na waandishi
habari wa Kenya, majuma mawili yaliyopita watu 12 waliuwawa katika tukio kama
hilo karibu na mahala hapo.
Post a Comment