kundi la watu wenye ulemavu wakiwa katika warsha hiyo |
Bw. Deus
Kibamba
MWENYEKITI wa jukwaa la
katiba nchini Deus Kibamba amesema kuwa pamoja na Tanzania kuwa na
mchakato wa kuunda katiba mpya zaidi ya mara nne sasa ila
mchakato wa sasa unaweza kusaidia kuwa na katiba nzuri zaidi
na kuwataka watanzania kutosusia mchakato huo wa kutoa maoni yao kwani
mwisho kuna nafasi ya kuipigia kura.
Kibamba aliyasema hayo
leo wakati wa mafunzo ya siku mbili ya maandalizi ya tamasha la mwaka la
azaki za kiraia warsha inayoendelea katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar
es Salaam.
Kwani amesema kuwa
katika mchakato wa sasa kuna sheria inayoongoza mchakato (CRA) pia kuna penyo
za Demokrasia ,hata kama ni kidogo (Sect 6(6) of CRA etc.
Kuna fursa ya
makundi kujiunda kama mabaraza ya katiba kuongoza mjadala wa mambo yaliyomo
katika rasimu ya taarifa ya tume juu ya waliyoyarekodi,pamoja na kuwa na bunge
maalum la katiba la aina tofauti ikiwa ni pamoja na katiba kupigiwa kura
na watanzania wote wenye umri wa mtu mzima na yawezekana kupata kura ya
hapana iwapo itaonekana kuburuzwa ama kura ya ndio kama maoni yao yatafika
sahihi.
Katika mchakato wa
katiba mpya asasi za kiraia zatakiwa kushiriki katika mchakato huo
pia kuonyesha kuvutia upande wowote katika utoaji wa
maoni yao.
Kuwawapo baadhi
ya watu wanatambua kuwepo kwa mchakato huo wa katiba ni wachache
na wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi huku sehemu kubwa ya watanzania
hawana uelewa wa kutosha juu ya mchakato huo.
Kuwa toka nchi ipate uhuru mwaka
1961 hadi sasa Taifa limepata kuwa na katiba 5 ambazo zimeundwa hivyo kama
tunatambua kuwa uelewa wa watanzania na ushiriki wao katika mchakato wa
katiba ni vema kueleweka zaidi.
Hivyo alisema kuwa
asasi za kiraia zinapaswa kuhakikisha zinafanya vema katika mchakato huo
ikiwa ni pamoja na kushiriki kutoa maoni yatakayosaidia kupata katiba
nzuri zaidi itakayoshirikisha maoni sahihi ya wananchi pasipo kuunda katiba
yenye sura isiyoeleweka katika katiba hiyo.
Alisema ni vema
wananchi wakatambua kuwa ni nini kitabadilika katika katiba hiyo mpya ambayo
mchakato wake unaendelea .
“Natambua kuwa
wapo wanaohofu mchakato huo kuwabana labda wenye mali nyingi kama ilivyokuwa
wakati wa azimio la Arusha na baadhi yao hata viongozi wa azaki za kiraia ama
wanasiasa ila bado nawaomba tusiogope kushiriki ….ila wito wangu kwenu wana
azaki kwa kila tunachokifanya kifanyike kwa maslahi ya Taifa na sio
maslahi binafsi “
Kibamba alisema kuwa
katika mchakato huo wa sasa unakwenda vizuri baada ya tume kujirekebisha
kasoro ndogo zilizokuwepo kwa kuondoa vitisho kwa wananchi
na sasa wananchi wanashiriki vema katika mchakato huo.
Japo kasi ni ndogo
zaidi kutokana na idadi ya kata zinazofikiwa katika wilaya husika
kuwa kata chache zaidi.
Alisema kuwa njia
ya simu kwa sasa imeanza kutumika kwa ajili ya kutoa maoni hayo na njia
nyingine kwa wananchi kutoa maoni yao kupitia mitandaa mbali mbali
ya mawasiliano njia ambayo azaki zinapaswa pia
kuhamasisha wananchi kushiriki kwa njia hizo kwa wale walioshindwa kufika
katika mikutano ya mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya
katiba.
Post a Comment