Kaimu Katibu Mkuu
katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Longinus Rutasitara (katikati)
akifafanua jambo wakati wa mkutano na Wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu
wa China na wadau wengine (hawapo pichani) kujadili misaada ya Serikali ya China
katika kuisadia Tanzania kutekeleza miradi mikubwa katika sekta kama vile
Kilimo, Miundombinu na Umeme. Wengine katika picha ni Maafisa Waandamizi kutoka
Tume hiyo.
Balozi Mbelwa Kairuki
(kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano na
ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi yake
mikubwa. Wengine katika picha ni Bw. Lin Zhiyong (katikati) Mwakilishi Mkuu
katika masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
hapa nchini na Bi. Fang Wang, Afisa kutoka Ofisi hiyo.Picha na Habari-Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa
Post a Comment