Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye amesema kwamba uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara na
Makamu Mwenyekiti Zanzibar utafanyika kesho tarehe 13 Novemba 2012.
Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,uliofanyika leo
asubuhi Kizota mjini Dodoma,Nape alizungumzia kufanikiwa kwa siku ya jana, baada
kila kitu kwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba.
Pia alizungumzia ratiba ya leo,ambapo kutakuwa na Taarifa
mbali mbali za kazi za chama,Taarifa za utekelezaji za ilani ya uchaguzi (Bara
na Zanzibar) itasomwa na Waziri Mkuu Mizengo Kayanda Pinda kwa upande wa
Tanzania bara na kwa upande wa Tanzania visiwani itasomwa na na Makamu wa Pili
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.Taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
pia zitasomwa leo.
Akizungumzia mabadiliko ya Katiba,alisema kumekuwa na
mafanikio sana baada ya mapendekezo yote kupitwa bila kupingwa,moja ya
mapendekezo ni kuwepo kwa Baraza la Ushauri la Wazee, pamoja kubariki
mapendekezo wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa watoke
wilayani.
Baada ya uchaguzi kutakuwa na mrejesho wa mijadala na kutoa
maazimio ya Mkutano Mkuu.
Post a Comment