Waasi wa kundi la M23
wakimshikilia mtu anayeshukiwa
mwanachama wa kundi la
FDLR.
SERIKALI ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo-DRC inasema kundi la waasi la M23 limeuwa watu 64 tangu
lilipouteka mji wa Goma uliopo mashariki mwa nchi hiyo wiki
iliyopita.
Shutuma hizo zilitolewa Jumatano na msemaji wa
serikali, Lambert Mende, ambaye anasema zaidi ya raia 220 wamejeruhiwa huko
Goma.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa
kutoa msaada pia wanaripoti kutokea vifo katika mji huo lakini hawajasema ni
nani anayehusika na vifo hivyo.
Mende pia alilishutumu
kundi hilo la waasi kwa wizi wa ngawira huko Goma kabla ya kundi hilo
kutangaza mipango ya kuondoka kwenye mji huo.
Mapema Jumatano mkuu wa jeshi la M23, Sultani
Makenga alisema majeshi yake yalianza kuondoka kutoka Masisi, mji uliopo
kilomita 50 kaskazini-magharibi mwa Goma na baadaye wataondoka Goma.
Shirika la habari la
Reuters lilisema waasi wa M23 pia waliondoka Sake, mji mwingine katika eneo
ambalo waliliteka. Mkuu wa kundi hilo Jean-Marie Runiga aliiambia Sauti ya
Amerika-VOA siku ya Jumanne kwamba majeshi ya M23 yataondoka Goma ifikapo Ijumaa
kama ishara ya nia njema.
Waasi hao wanasema
watarudi nyuma kilomita 20 nje ya Goma lakini wataacha kiasi cha wanajeshi 100
kwenye uwanja wa ndege mjini humo.

Post a Comment