Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Baraza la
Wataalam wa Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini leo jijini Dar es
salaam.
Mwenyekiti
wa Baraza la wataalam wa kurekebisha upeo wa macho kuona nchini Adam Simbeye
(kulia) akiwaeleza wajumbe malengo ya baraza hilo ya kusimamia, kudhibiti na
kuratibu utoaji wa huduma bora za macho nchini yanayofanywa na baraza hilo kwa
mujibu wa sheria ya Optometria Na.12 ya mwaka 2007. Kushoto ni Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi.
Wajumbe wa
Baraza la Wataalam wa Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini wakiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (Katikati)
mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo leo jijini Dar es
salaam.
Waziri wa
Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) na mwakilishi wa Shirika
la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) kwa pamoja wakisaini nyaraka za
kukabidhi magari 9 ya kubebea wagonjwa na pikipiki 107 kwa ajili ya kupelekwa
katika maeneo mbalimbali kusaidia huduma za afya.
Mwakilishi
wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) akimkabidhi funguo za
gari la kubebea wagonjwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi
leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akimkabidhi funguo za gari
la kubebea wagonjwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe Dkt.Archard
Rwezahura (katikati) leo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia makabidhiano hayo
ni mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam
Khan.Picha na Aron Msigwa -
MAELEZO.
Post a Comment