LICHA ya waasi wa M23
kutangaza kujiondoa kwenye mji wa Goma, Umoja wa Mataifa unasema waasi hao
hawajaonesha dalili ya kuondoka kabisa na umetoa wito kwa mataifa ya kigeni
kutojihusisha na mgogoro kwenye eneo hilo.
Umoja wa Mataifa
unatarajiwa kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa kundi la waasi wa M23 na
vile vile watu wanaowaunga mkono kutoka nje.
Kwenye azimio
lililopitishwa kwa kauli moja na Baraza la Usalama, Umoja huo umewataka waasi wa
M23 kuweka silaha zao chini na kuacha mapigano mara moja na pia kuwaachilia
watoto wanaohudumu kwenye kundi lao kama wapiganaji.
Likionesha wasiwasi wake
kufuatia taarifa za mauaji, ubakaji na kuajiriwa watoto kwenye kundi la M23,
Baraza la Usalama limeelezea nia ya ya kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi hilo
na watu wanaoaminika kuliunga mkono.
Miongoni mwa vikwazo
hivyo ni kupiga marufuku ya uuzwaji wa silaha kwa makundi ya waasi wa
Kongo.
Serikali ya Kongo ndiyo
yenye jukumu la kulinda watu wake
Marais Yoweri Museveni
wa Uganda (kushoto), Joseph Kabila wa DRC (katikati) na Paul Kagame wa Rwanda
katika mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu juu ya mzozo wa Kivu ya Kaskazini,
Novemba 2012.
Vile vile Umoja wa
Mataifa umeitaka serikali ya Rais Joseph Kabila kuendesha uchunguzi na
kuwaadhibu waliohusika na uhalifu huo, kwani "usalama na amani ya Kongo ni
jukumu la kwanza la serikali hiyo."
Msimamo huo unafuatia
lawama dhidi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo
(MONUSCO) ambacho hakikuzuwia kutekwa kwa mji wa Goma na waasi wa M23 wiki mbili
iliopita.
Baraza hilo
limeyatahadharisha makundi yote ya wapiganaji katika mashambulizi yao dhidi ya
walinda amani wa MONUSCO na raia wa kawaida. Baadaye, Baraza la Usalama
lilipitisha azimio linaloidhinisha ripoti ya wataalamu kuhusu
Kongo.
Mataifa ya kigeni
yalaumiwa
Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekanbi, Hillary Rodham Clinton.
Akizungumza na DW mjini
New York, Naibu Balozi wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa, Olivier Nduhungirehe,
alisema nchi yake inakubaliana na hatua hiyo ya Umoja wa Mataifa, lakini
aliendelea kukanusha kuhusika kwa nchi yake na mzozo wa Kongo.
"Rwanda siyo chanzo cha
mzozo wa Kongo na haijihusishi hata kidogo.
Tumeshangazwa sana na
msimamo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono ripoti ya kundi la
wataalamu inayoelezea kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23, bila ya Baraza
hili kuhoji mfumo wa uchunguzi, ushahidi na tuhuma za wataalamu hao dhidi ya
Rwanda." Alisema Balozi Nduhungirehe.
Balozi wa Jamhuri ya
Kodemokrasia ya Kongo nchini Ufaransa, Ileka Atoki, alielezea msimamo wa nchi
yake kwamba inataka viongozi wa Rwanda waliotajwa kwenye ripoti hiyo wawekewe
vikwazo.
"Ushahidi wa watu na
vifaa umetambuliwa na Umoja wa Mataifa kuthibitisha kuvamiwa kwa Kongo na nchi
ya Rwanda.
Mbali na hayo, Rwanda
inaendelea kukiuka marufuku ya Umoja wa Mataifa ya kutowapa silaha wapiganaji na
kusababisha hali mbaya ya kiutu kwenye mkoa wa Kivu ya
kaskazini.
Kutokana na mauwaji
hayo, serikali ya Kongo na jumla ya raia wake wote wanasubiri kuona hatua kali
zikichukuliwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya wahusika wa machafuko
hayo."
Baada ya azimio hilo la
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kiongozi wa Kamati ya Vikwazo vya Umoja
huo anatarajiwa kuwasilisha orodha ya majina ya watu watakaowekewa vikwazo
mwishoni mwa wiki hii.
Duru za kuaminika za
Umoja wa Mataifa zimeimbia DW kwamba Umoja huo utafuatilia kwa karibu
kutekelezwa kwa matokeo ya Mkutano wa Marais wa Nchi za Maziwa Makuu kuhusu
usitishwaji mapigano na kuondoka kwa waasi kwenye mji wa Goma.
Mataifa ya Magharibi
yaendelea na diplomasia
Waasi wa M23 wakipiga
doria kwenye mji wa Goma.
Hatua hii inakuja katika
wakati ambapo Marekani, Uingereza na Ufaransa zinaendesha juhudi maalumu za
kidiplomasia katika mataifa ya Kongo, Rwanda na Uganda ili papatikane suluhisho
la mzozo wa hivi sasa kwenye mkoa wa Kivu ya Kaskazini.
Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekani, Hillary Clinton, amewatolea wito viongozi wote wa eneo la Maziwa
Makuu kusitisha kuwasaidia waasi wa M23.
Akigusia ukweli kwamba
kiasi cha watu 285,000 wameshayakimbia makaazi yao tangu waasi hao waanze
kuelekea mjini Goma mwezi Aprili, Clinton amesema wengi wa watu hao wanahitaji
msaada wa dharura na akawataka waasi kuacha mashambulizi na kujiondoa moja kwa
moja mjini Goma.
"Tunawatolea wito
viongozi na serikali zao katika eneo zima kusita na kuzuia msaada wowote kwa M23
kutoka ndani ya mipaka za nchi zao." Alisema Clinton katika kile kinachotajwa
kuwa ni kauli nzito zaidi kuitoa tangu mzozo huu kulikumba eneo la Maziwa Makuu

Post a Comment