Watanzania
waishio Ujerumani kufanya hafla ya kumuaga Mhe,Balozi Bw.Ahmada Ngemera
! Jumamosi
08-December 2012 mjini Berlin,Ujerumani.
Umoja wa
Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania
wote wanaoishi
ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya afla ya
kumuaga Mheshimiwa
balozi, Ahmada Ngemera, ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi.
Mhe.
Balozi bwana Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na
watanzania wanaoishi
ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi Bw.Ahmada Ngemera kwa kuwa karibu
sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho
watanzania
wa
ujerumani wanachokiita
kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi
ujerumani,ambapo Mhe. Balozi, Ngemera na msaidizi wake
Mhe.Bw.Ali Siwa wahamua kuhamasisha watanzania waishio Ujerumani kuungana katika kila
hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu
ambacho mabalozi wengi walishindwa
kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya ujerumani wa watanzania wanaishi katika
miji mbali mbali,lakini kazi hiyo ya kuwaungunganisha watanzania, Balozi Bw.Ahmada Ngemera na
Msaidizi wake Bw.Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia watanzania wote waishio Ujerumani na
kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda ya juhudi zao ndipo
kukazaliwa Umoja wa
waTanzania Ujerumani.(UTU) Umoja ambao ni chombo cha
watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia
.
UMOJA NA
MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:
TUNAWAOMBA
WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO
WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA AFLA HII,
TUNAOMBA
MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU
kwa
kupitia Account : Union of
Tanzania in German e.V.
VR Bank
Rosenheim-Chiemsee AG
Konto-No.:
59641 BLZ:
71160161
Verwendungszweck:
„Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera
Pia unaweza
kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com
Post a Comment