Uongozi
wa klabu ya Young Africans umemalizana na mchezaji wake wa zamani John Njoroge
aliekua na madai yake ya kuvunjwa mkataba wake miaka miwili iliyopita, hali
iliyompelekea Njoroge kuishtaki Yanga FIFA na jana jioni Uongozi umemalizana
nae.
Akiongea
na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz katibu mkuu
wa Young Africans Lawrence Mwalusako amesema wamefikia mwisho juu ya suala na
hilo ambapo jana jioni Njorogen alipokea pesa aliyokua akidai klabu ya
Yanga.
Awali
tulitangulia kumlipa tsh milioni 4 ambapo alitaka kumaliziwa pesa yake kwa
pamoja, na jana klabu ya Young Africans ilimalizia kumlipa tshs milioni 14 kama
alivyoelekeza na hivyo Yanga kuwa imemlipa jumla ya tshs milioni 17 alizokuwa
anadai alisema 'Mwalusako'
Mchezaji
John Njoroge aliyejiunga na Young Africans akitokea Tusker FC ya Kenya amelipwa
jumla ya tshs milioni 17 ambazo tayari amedhibitisha kuzipokea na kutuma
kiambatanisho cha malipo FIFA
John
Njoroge alisajiliwa Young Africans mwaka 2008 kwa mkataba wa miaka miwili kabla
ya kuongezewa tena mkataba wa mwingine ambao ulilkua na utata hatua iliyopelekea
Njoroge kwenda kuishitaki Yanga FIFA.
Kufuatia
hatua hii Uongozi wa Young Africans unawashukuru wapenzi, washabiki na wanachama
wake kwa kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho uongozi ulikuwa
unalishulikia suala hili.

.jpg)

Post a Comment