Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haji Omar Kheir (katikati) akiwa katika
Kikao ambacho kinajadili Mkutano wa Jumuia ya Afrika ya Utumishi wa Umma na
Uongozi (AAPAM) utakao fanyika Zanzibar kuanzia tarehe 12-16 Novemba huko
Zanzibar Beach Resort.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haji Omar Kheir (kulia) akielezea kitu
katika Kikao ambacho kinajadili Mkutano wa Jumuia ya Afrika ya Utumishi wa Umma
na Uongozi (AAPAM) utakao fanyika Zanzibar kuanzia tarehe 12-16 Novemba huko
Zanzibar Beach Resort.
Na Maelezo Zanzibar
01/11/2012
Zanzibar inatarajiwa
kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 34 wa Jumuiya ya Kiafrika ya Utumishi wa Umma na
Uongozi (AAPAM) utakaofanyika kuanzia Tarehe 12-16 mwezi huu huko katika Ukumbi
wa Zanzibar Beach Resort nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akizungumza na waandishi
wa Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji
Omar Kheri huko Ofisini kwake Vuga leo amesema kuwa Mkutano huo uatasaidia
katika kuitangaza Zanzibar nje ya Nchi.
Amesema kuwa kutangazwa
huko kutasaidia zaidi katika kuimarisha utalii wake ambao unasaidia sana katika
uchumi wa Zanzibar ambapo asilimia 80 ya fedha za kigeni zinapatikana kutoka
sekta hiyo.
Mbali ya hivyo
wajasiriali wa Zanzibar nao kwa upande wao watapata fursa ya kutangaza bidhaa
zao kutokana na idadi kubwa ya washiriki kutoka sehemu mbali mbali za nchi za
Kiafrika na Jumuiya ya Madola.
Amesema kuwa zadi ya
Wajumbe 400 kutoka nchi Jumuiya Wanachama wanatarajiwa kushiriki Mkutano huo
ambapo watatafakari juu ya mwenendo wa Utumishi unavyokwenda katika Taasisi
mbali mbali Afrika na Duniani.
Akielezea juu ya malengo
makuu ya Mkutano huo Waziri Kheri amesema kuwa ni kubadilishana uzoefu katika
masuala ya kiutumishi wa Umma na utawala pamoja na kuandaa mipango ya
kukabiliana na changamoto zinazoikumba Sekta ya Utumishi wa Umma na
Uongozi.
Amewataka Wananchi
kujipanga vyema kuutumia Mkutano huo kama fursa nzuri ya kujifunza ili kupata
maendeleo ya baadaye na kutoa kila aina ya mashirikiano ya kufanikisha Mkutano
huo.
Aidha Waziri Kheri
amewata wananchi pia kudumisha usalama ili wageni ambao watashiri katika Mkutano
huo kufanya shughuli zao bila ya vikwazo na bughudha yoyote
ile.
Mkutano kama huo mwaka
jana ulifanyika Nchini Malawi ambapo Mwaka huu hapa Zanzibar Mkutano huo
unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt.Ali Mohamed Shein.


Post a Comment