Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZUNGU AKANUSHA TUHUMA ZAKE ZA KUKAMATWA NA TAKUKURU




Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu (kushoto) akikanusha kukamatwa na rushwa na takukuru wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bunge mjini Dodoma leo.Kulia ni Mbunge wa Mafia Abdurahman Shah.

Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu leo amekanusha kukamatwa na Rushwa na takukuru kwenye mkutano mkuu wa jumuia ya wazazi uliofanyika juzi. Zungu amesema kuwa magazeti yamekaririwa kupotosha ukweli kuwa yeye Zungu alikuwa amekamatwa na Rushwa.

Amefafanua kuwa yeye alisimamishwa na maafisa wa Takukuru na kupekuliwa gari lake na kuchukua simu zake kwa ajili ya uchunguzi zaidi na siyo kukamatwa na maafisa hao Zungu ametaka magazeti hayo kuandika katika kurasa za kwanza habari za kukanushwa kwa kukamatwa kwake kinyume cha hapo atachukua mkondo wa sheria mahakamani.

Amedai kuwa habari hizo zimesumbua jamii ya Tanzania, ndugu zake na wapiga kura wake wa jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam ukizingatia kuwa yeye ni kiongozi wa umma. Amesema kuwa habari hizi zimetumika kisiasa sana kwa nia ya kumchafua yeye asipite ujumbe wa NEC ya CCM kupitia jumuia ya wazazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top