Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

PAMBANO LA CHEKA NA MJERUMANI LAOTA MBAWA



LILE pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa ngumi nchini Tanzania na Ujerumani kati ya Francis Cheka na Benjamin Simon wa Ujerumani limefutwa.



Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo na Rais IBF Africa, Onesmo Alfred McBride Ngowi unasema kuwa pambano hilo limefutwa kufuatia mpinzani wa Cheka kuumia.



“Mpinzanai wa bondia Francis Cheka toka Ujerumani, Benjamin Simon ambaye walikuwa wapambane tarehe 18 Decemba kugombea mkanda wa IBF wa mabara ameumia na mpambano wao umefutwa,” ilisema sehemu ya taarifa hizo ya paraghafu mbili.



Rais IBF Africa, Onesmo Alfred McBride Ngowi amesema kuwa taarifa za kufutwa kwa pambano hilo amezipokea kutoka kwa Meneja wa Simon, Robert Dolle ambaye naye ni bondia pia ameiarifu IBF kuwa walikuwa wanangoea kujua kama kweli hataweza kucheza ndio watoe taarifa hiyo.



Pambano baina ya wababe hao lipangwa kufanyika tarehe 18 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani.


Tayari bondia Francis Cheka alishasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la “Iron Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde yanayowasulubu wapinzania wake.



Bondia Benjamin Simon ana rekodi ya mapambano 24 ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza mapambano 6.


Akimwandikia “Eva Rolle” wa kampuni ya “Primetime Event Management” ya Ujerumani ambaye ndiye promota wa mpambano huo, mwenyekiti wa ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa watakaosimamia mpambano huo.


Endapo mpambano huo unefabyika ingekuwa ni mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C) na mpambano wao ungekuwa wa hindani mkubwa.


Mshindi katika mpambano huo angeingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top