Mkuu wa usalama wa kidiplomasia wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Eric Boswell na maafisa wengine watatu wa wizara hiyo wamejiuzulu kutokana na ripoti kuhusu mashambulizi ya Septemba 11 dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi kugundua mapungufu makubwa katika hatua za kiusalama kwenye wizara hiyo.
Taarifa ya kujiuzulu kwa Boswell imetolewa na Msemaji wa wizara hiyo Victoria Nuland.
Ripoti hiyo ina mapendekezo 29 ambayo yote yamekubaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi Hillary Clinton.
Awali katika barua yake kwa kamati ya bunge la Marekani, Clinton alisema ameielekeza wizara yake kutekeleza haraka yale yaliyomo kwenye ripoti hiyo.
Maafisa wanne wa Marekani waliauwa katika shambulio hilo, akiwemo aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens.