Kutokana na ushindi huo wa magoli matano yaliyofungwa na Juan Mata, Branislav Ivanovic, Victor Moses, Eden Hazard na Fernando Torres Chelsea imekata tiketi ya kucheza michuano ya robo fainali za michuano ya Capital Cup ambapo itakutana na timu ya Swansea.
Nusu fainali nyingine itakuwa ni kati ya Bradford na Aston Villa ambayo itachezwa kati ya tarehe 7 na 21 mwakani.
Wakati huo huo vilabu saba vya Uingereza vinasubiri droo ya Ligi ya mabingwa na Bara la Ulaya baadae leo.
Manchester United, Arsenal na Celtic zinasubiri kujua wapinzania wao wakati katika hatua ya mchujo wa 16 bora katika Ligi Kuu ya Mabingwa Bara Ulaya, huku Liverpool, Tottenham, New Castle na Chelsea zilisubiri droo ya 32 bora bara la Ukaya.