![]() |
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum Ally akizungumza na vyombo vya habari. |
ABIRIA na wananchi wanaotumia kivuko cha MV. SAMAR wamepinga
vikali agizo la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizebar la kuamuru
kusitishwa kwa huduma ya usafiri wa kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya
Mwanza mjini na Kamanga Wilayani Sengerema hali iliyopelekea wananchi kupinga
vikali hatua hiyo ya Naibu Waziri na Serikali.
Wananchi na abiria hao wamesema kwamba kauli hiyo ya
Naibu Waziri Dkt.Tizebar aliyoitoa hivi karibuni wakati wa kuipokea treni ya
abiria ya kutoka Jijini Dar es salaam hadi Jijini Mwanza kuwasili kwa mara ya
kwanza tangu kuanza kazi Desemba 9 mwaka huu baada ya kusitisha safari zake kwa
miaka mitatu kwa madai kuwa wamezuia njia ya reli iendayo bandarini huku madai
hayo yakionekana kupingana na Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini waliodai
kuwa kwa sasa hawahitaji huduma ya Treni kufika Bandari hiyo na ni miaka zaidi
ya kumi Treni kupita na kufika Bandari hiyo ya Mwanza
Kaskazini.
Akizungumza na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Kampuni
ya Meli ya MV. SAMAR Salum Ally alisema kwamba agizo la kusimamisha huduma na
kuhamia eneo la maegesho ya Meli za Marine Service huku kukiwa hakuna
matayarisho ya barabara ya magari kuingia na kutokea,abiria na daraja la meli
hiyo kuweka nanga ili kuruhusu abiria na magari kupita kirahisi kama ilivyo
kwenye eneo kilipokuwa kikitolea huduma
awali.
Salum amesema kwamba alipokea barua ya kwanza ya
Mamlaka ya Bandari ya Kaskazini (PTA) Desemba 11 mwaka 2012 yenye kumb.MN/2/3/04
iliyosainiwa na Mkuu wa Bandari hiyo Mhandisi Josephat Mutalemwa huu ikisomeka
kwamba ‘AGIZO LA NAIBU WAZIRI LA KUHAMISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO
NA KUELEKEA NDANI ZAIDI YA BANDARI YA KASKAZINI’ ikiwa ndani ya wiki tatu za
kutekelezwa kwa agizo hilo.
![]() |
Barua ya kwanza. |
Ameongeza kuwa wakati akitafakali juu ya uamuzi huo wa
barua hiyo na Agizo la Naibu Waziri Dkt.Tizebar,Kabla ya wiki moja kumalizika
ghafla akapokea barua nyingine tena ya pili ambayo pia ikitolewa na PTA Desemba
19 mwaka huu na ikisainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari T.S.Akile iliyosemeka
'KUSITISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO NA KUELEKEA ZAIDI NDANI YA BANDARI
YA KASKAZINI' Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (PTA) inakutaka kusitisha mara
moja shughuli za kupakia na kushusha abiria na mizingo kuanzia sasa hivi (Leo
Desemba 19 mwaka huu).
Kufatia hatua hiyo hali ilikuwa tofauti kwa wananchi
na abiria na kuanza kurusha mameno na kauli kali za kupinga hatua ya
PTA,Serikali na Agizo la Naibu Waziri Dkt. Huku Mkurugenzi wa SAMAR alidai kuwa
ameheshimu kauli ya Waziri na agizo la barua za PTA, akidai kuwa amekuwa
akiilipa PTA kiasi cha shilingi milioni 2 kwa mwezi ikiwa ni makubaliano baada
ya kuomba kutumia eneo hilo na kupitia Meli zake amekuwa pia akiliingizia
shirika hilo kiasi cha zaidi milioni 70 kwa mwezi kwa huduma ya Bandari ya
Mwanza Kaskazini na Kusini.
Mbali na kuiingizia PTA mapato hayo, kampuni hiyo imekuwa akisaidia wanawake wajane zaidi 60 kiasi cha shilingi 600,000 kwa mwezi waliopo eneo la Kamanga huku serikali ya Kijiji hicho cha Kamanga kikiingiza kila siku kiasi cha elfu 40,000/= ikiwa ni huduma za wananchi wanaotumia vyoo katika eneo la kugota Meli ya MV. SAMAR huku wanafunzi wote wakipita bure katika kivuko hicho wakiwemo wazee wa zaidi ya miaka 70 na mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 8 kila siku ya huduma wa Meli hiyo.
Mbali na kuiingizia PTA mapato hayo, kampuni hiyo imekuwa akisaidia wanawake wajane zaidi 60 kiasi cha shilingi 600,000 kwa mwezi waliopo eneo la Kamanga huku serikali ya Kijiji hicho cha Kamanga kikiingiza kila siku kiasi cha elfu 40,000/= ikiwa ni huduma za wananchi wanaotumia vyoo katika eneo la kugota Meli ya MV. SAMAR huku wanafunzi wote wakipita bure katika kivuko hicho wakiwemo wazee wa zaidi ya miaka 70 na mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 8 kila siku ya huduma wa Meli hiyo.
![]() |
Kivuko hicho cha MV.SAMAR. |
Post a Comment