![]() |
| BAADHI YA AKINA
MAMA WASAMARIA WEMA WA TANANGOZI IRINGA WAKIJARIBU KUMPEPELEKA MMOJA WA
MAJERUHI WA AJALI ILIYOTOKEA DESEMBA 4,2012 HUKO TANANGOZI IRINGA LIKIHUSISHA
TOYOTA RAV 4 T 770 BMP LILILOINGIA NYUMA YA TRAILER T 566 BNQ AMBAPO WATU
WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWA WAKITOKEA DAR KWENDA MBEYA WALIFARIKI PAPO
HAPO 6:BAADHI YA WASAMARIA WEMA WAKITOA MOJA YA MAITI KUTOKA KATIKA GARI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA DESEMBA 4,2012 WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWEMO KATIKA GARI HILO WALIFARIKI PAPO HAPO(PICHA ZOTE NA MISANJO LIVIGHA (MLALAHOI ALWATAN WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM |
GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN
NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA
RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA
FAMILIA MOJA PAPO HAPO WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV
4
Na Francis
Godwin
Ajali mbaya imetokea mkoani
Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja
pamoja na mfanyakazi wa ndani.
Ajali hiyo imetokea katika
eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa
kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane
mchana
Kwa mujibu wa mashuda wa
tukio hilo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4
lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma. Huku chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha
kwa mwendo kasi wa dereva wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na
kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa
nyuma.
Kwa mujibu
wa mashuda wa tukio hilo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo
aina ya Rav 4 kuendesha kwa mwendo kasi na kushindwa kulimudu na kulipalamia
lori kwa nyuma na kuwa gari hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda
Kyela mkoani Mbeya.
Hivyo katika ajali hiyo
abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika
gari hiyo pamoja na watoto hao kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa
katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majina ya waliokufa ni
pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa
familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy
Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel
huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa
Iringa.






Post a Comment