MSANII
wa filamu nchini, Sajuki alidondoka jukwaani juzi wakati akijaribu kuwasalimia
mashabiki wake waliofurika kumtazama kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,
Arusha.
Sajuki
ambaye jina lake halisi ni Juma Said Kilowoko alikuwa akisumbuliwa na matatizo
ya kupungukiwa dawa na kulazimika kwenda kutibiwa nchini India.
Mwingizaji
huyo alipanda jukwaani katika tamasha la lililowahusisha wasanii wa filamu na
muziki, lakini ndoto yake ya kusalimia mashabiki wake
hakuwezekana.
Mara
baada ya kukabidhiwa kipaza sauti Sajuki alitamka neno moja ”ahhh" na kudondoka
chini na wasanii wenzake walimsaidia kuinuka na kumuondoa jukwaani
hapo.
Akizungumza
na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki alisema hali
yangu si nzuri kwani nahishiwa nguvu na anahitaji matibabu
zaidi.
”Kaka
hali yangu si nzuri kabisa naumwa, sijisikii vizuri,” alisema Sajuki huku
akionekana mnyonge zaidi...
Hata
hivyo, mashabiki wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali hiyo na
kushutumu wasanii walioamua kumtumia ili wapate fedha ihali mwenzao ni
mgonjwa.
“Hawa
watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu huyu mtu anaumwa, badala ya kumwacha
apumzike wenyewe wanamzungusha bila ya kujali afya yake,” walisema mashabiki
hao.
Post a Comment