ASKOFwa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Alex Malasusa amesema hapendezwi na
matumizi ya nguvu yanayofanywa na Jeshi la Polisi hata kwenye migogoro
ya wanafunzi wa shule za msingi.
Kauli hiyo iliitolewa
jijini Dar es Salaam leo, Askofu huyo, wakati akitoa ujumbe wa amani wa Siku ya
njema ya kuzaliwa Yesu (Christmas).
Malasusa alisema matumizi
ya nguvu tena kwa kuwapiga mabomu watoto hao wa shule za msingi inamtia hofu kwa
kuwa haelewi baada ya miaka kumi watoto hao watakuwa wamejifunza
nini.
“Wakati nikiwa mtoto
nilizoea kuwaona askari wakitembea na fimbo lakini siku hizi matumizi ya silaha
yamekuwa yakiongezeka sehemu mbalimbali”alisema.
Askofu Malasusa alisema
utasikia baadhi ya watu wanasistiza kudumishwa kwa amani na utulivu lakini hao
hao wanakuwa wakwanza kuharibu amani hiyo huku wakitegemea
jeshi.
Aliwakumbusha viongozi kuwa
ili amani indelee kudumu nchini ni lazima wajenge tabia ya kuvumiliana katika
masuala mbalimbali, kwani amani hailindwi kwa silaha bali ni utashi wa
watu.
Akifafanua zaidi katika
ujumbe huo wa Christmas, alisema amani ni lazima iwe tabia ndani ya maisha ya
kila mtu na inapokosekana watu wote wasiwe na furaha.
Alisema kuna familia nyingi
ambazo amani kati ya mume na mke imetoweka kutokana na kushuka kwa
maadili.
“Kuna ndoa nyingi zimekuwa
za majuto kwa sababu watu wengi wameshindwa kutii amri ya mungu”alisema
Malasusa.
Askofu Malasusa alisema
wapo wengi wanaotaka kuwa juu kimaendeleo, hilo siyo baya bali kikubwa ni
kumuweka Yesu moyoni.
Post a Comment