Mafahali mawili wanaotegemea kuzichapa tarehe 25, 2012 kugombea
mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati
Mtanzania Francis Cheka na Mmalawi Chiotcha Chimwemwe nusura wazichape kavukavu
wakati wa upimaji uzito na mkutano wa waandishi wa habari katika hoteli ya
nyota 5 ya Naura Springs, jijini Arusha leo tarehe 25 Desemba
2012. Hii ni mara ya kwanza kwa ngumi za kulipwa kupewa hadhi kubwa
kama hiyo ya kuwekwa kwenye hoteli ya nyota tano (5) hapa Tanzania.
Wawili hao walikuwa katika hoteli hiyo ya kifahari ya Naura
Springs inayomilikiwa na bwana Felix Mrema anayemiliki mahoteli lukuki katika
jiji la Arusha na Moshi ambazo ni Naura Springs Hotel, Impala Hotel, Ngurudito
Hotel, Impala Moshi na Livingstone Hotel za Moshi!
Mpambano huo uliopewa jina la “Vurumaini chini ya Mlima
Meru”umekuwa ni gumzo katika jiji la Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Manyara
pamoja na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda na unaandaliwa na
kampuni ya kizalendo ya Green Hills (T) Limited inayomilikiwa na bondia wa
zamani wa taifa katika ngumi za ridhaa na kuloipwa George Andrew na familia
yake.
Aidha, watalii wengi walioko katika jiji la Arusha wakati huu wa
sikukuu ya Xmas wameonyesha nia zao za kuliangalia pambano hili na wengine
wameshakata tiketi tayari kuingia katika ujwanja wa Sheik Amri Abeid
kuwashughudia mafahali hao wawili wakitoana jasho. Chiotcha mwana wa
Chimwemwe mwanajeshi wa ngazi ya Luteini Usu katika jeshi la Malawi amepania
kulibeba juu taifa lake lililoko pembezoni mwa ziwa Nyasa kwa kumwonyesha
Francis Cheka kuwa ngumi zinaendana na ushupavu.
Chimwemwe anadai kuwa hakuja Tanzania kutalii kama walivyo
watalii wengine bali alikuja kuwakilisha nchi yake aipendayo ya Malawi na
kurudi kwao na mshipi wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati. Alisema kuwa kushinda kwake sio kitu cha kubahatisha ila ni
uhakika.
Naye Francis mwana wa Cheka, Mtanzania aliyeipeperusha vyama
bendera ya taifa hili katika mapambano mengi bila kuzivunja nyoyo za mashabiki
wa ngumi nchini alisema kuwa “Mwache Mmalawi huyo ajifurahishe tu kwani
hajui kinachongojea ulingoni”
Cheka aliyejizolea sifa kemkem kati ya mabondia wa kitanzania
aliendelea kusema kuwa yeye sio mzungumzaji sana ila ngumi zake ndizo
zitakazozungumza siku ya tareeh 26 Desemba, 2012.
“Asifikirie kuwa ngumi ni kupiga makelele tu na ukashinfa”
alisema Chelka akimwangalia Chimwemwe wakati alipokuwa anajigamba kwa sifa
kemkem!
Mpambano huo wa kukata na shoka unakuja wakati ambako Arusha
imekuwa ni jiji na linataka kutumia mapambano mengi ya ngumi ya kimataifa
kukuza hadhi ya jiji hilo kama “Geneva ya Afrika” kutokana na mandari
yake na mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika katika jiji hili.
Francis Cheka anakutana na Chimwemwe baada ya kuutema mkanda
wake wa IBF wakati alipokutana na Karama Nyilawila kugombea mkanda mwingine
mbali na IBF hivyo kuupoteza ubingwa wa IBF. Cheka amepania kuuchukua tena
mshipi huo na kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ni moto wa kuotea mbali!
Mpambano huo utahudhuriwa na viongozi wengi wakiongozwa na Meya
wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo pamoja na wageni wengi wanaofanya
kazi kwenye mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mahakama ya
kimataifa ya wahalifu wa kivita wa Rwanda, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na
Kati, ILO, UNICEF, WFP na nyingine nyingi.
Aidha watalii wengi wameacha kwenda mbugani siku ya pambano ili
washughudie wenyewe ni nani zaidi kati ya Cheka na Chimwemwe., Pamabano
hilo linaratibiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) chini ya Rais
wake Onesmo Ngowi na kupewa baraka zote na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa
(IBF).
Waamuzi wa pambano ni:
Onesmo Ngowi - Kamishna Mkuu, Roman Chuwa ambaye ndiye Kamishna
wa TPBC mkoa wa Arusha –(Kamishna Mkuu Msaidizi), Nemes Kavishe (Refarii),
Boniface Wambura – (Jaji), Gallous Ligongo –(Jaji), Mark Hatia –(Jaji).
on Tuesday, December 25, 2012
Post a Comment