
Penina huyo katika pozi
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
MCHEZA filamu za kibongo Tanzania,
Jenifer Raymond, maarufu kama Penina, amesema baada ya kubadili dini na kuwa
Muislamu, ametulia na kuangalia zaidi maisha yake ya ndoa aliyofunga na mwarabu
mmoja jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalumu.
Penina akiwa na msanii
mwenzake Mshindo Jumanne
Penina aliyewika zaidi katika
sanaa, alitangaza kubadili dini hiyo kwasababu ya kutaka ndoa ya mwarabu
mmoja.
Akizungumza na Handeni Kwetu
mapema leo, Penina alisema aliamua kubadili dini kwa ridhaa yake akiwa na lengo
la kuacha usichana wake.
Alisema katika maisha yake ya ndoa na mume wake huyo, ameweza kuvaa vyema uhusika wake, ingawa soko la sanaa bado analitendea, huku akiongeza kuwa u siri wa ndoa yao unatokana na kuogopa media zinavyoweza kuingilia kati na kuvuruga mapenzi ya watu.
Penina kama kawaida yake
“Nimeamua mwenyewe kubadili dini
na kuolewa na mwarabu nikifuata dini yake ya Uislamu, lakini siri ilikubwa kubwa
kwasababu bila hivyo ndoa yetu inaweza kuvunjika hasa kama wote tutakuwa wepesi
kusoma na kuvifanyia kazi vichwa vya habari.
Penina alicheza filamu nyingi
ikiwamo hiyo ya Penina aliyocheza na marahemu Steven Kanumba, Dar es Salaam na
nyinginezo nyingi zilizompa umaarufu hapa nchini.
Post a Comment