Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Aunty Ezekiel Akiri Kufurahia Maisha ya Ndoa Japo Ndio Anaanza

Aunt Ezekiel akiwa na Mumewe wakipata maakuli huko Dubai
MSANII mahiri wa filamu ambaye kwa sasa ni mke wa mtu Aunty Ezekiel, amerudi hivi karibuni kutoka Dubai wanakoishi na mume wake ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa maisha ya ndoa kwa upande wake yako safi kwani ndiyo kwanza anaanza hivyo hajajua machungu yake wala matatizo yake.

Alisema kuwa anaamini kutokana na upendo wa dhati alionao kwa mume wake ndoa yake itakuwa yenye furaha siku zote kama ilivyo sasa kwani wanapendana kupita maelezo.

“Kwa kweli nikisema sasa nitakuwa muongo kwani ndiyo kwanza nimeingia na unajua kwamba sina uzoefu wowote katika ndoa, lakini kwa muda huu nimekuwa naona yako pouwa kwa sababu upendo haujapungua ndiyo kwanza unaongezeka,” alisema.

Hata hivyo kwa upande wa filamu alisema kuwa hajarudi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo kwani kwa mwaka huu ndo amefunga ukurasa na hapo mwakani Mungu akijalia atafanya mchakato wa kurudi upya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top