Katika
kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano ya Afrika
Azam FC imefanya usajili wa wachezaji nane wapya katika kipindi hiki cha dirisha
dogo
Azam FC ambayo ilikuwa na wachezaji wanne wa kimataifa kufuatia
George Odhiambo kuondolewa mapema kutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza
wachezaji Ibrahim Shikanda na Joseph Owino na hivyo kuwa na nafasi tatu za
kimataifa
Azam FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki
wa kati wa Harambee Stars na klabu ya Tusker FC, Kiungo mshambuliaji wa Harambee
Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezaji bora wa
mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony.
Pia
Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu
akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli
nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo
haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya
CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi
Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa
Sugar katika mzunguko wa kwanza.
Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi
pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili
kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
Usajili huu umesimamiwa na
mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu
kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa
kuanza januari 20.
Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko
wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na
imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare
1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
Azam FC inatarajia
kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja
kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.
Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza.
Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.
Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.
Post a Comment