![]() |
Cannavaro |
Na Princess
Asia wa Bin Zubeiry
NAHODHA wa
Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kung’ara katika Kombe la Mataifa ya
Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mjini Kampala,
Uganda.
Katika
michuano hiyo, Cannavaro ambaye pia Nahodha wa Zanzibar, aliiongoza timu hiyo
kushika nafasi ya tatu katika michuano iliyoanza Novemba 24 na kufikia tamati
Desemba 8, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen ametaja
kikosi cha wachezaji 24, ndani yake akiwatema chipukizi aliokuwa akiwakomaza
kwenye timu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Edward Christopher, wote wa SImba
SC.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen
alisema kikosi hicho kitaingia kambini keshokutwa kwa ajili ya kujiandaa na
mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia, Chipolopolo
itakayochezwa Desemba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mbali na
Cannavaro na Aishi Mangula, nyota wengine wapya walioitwa katika kikosi hicho ni
pamoja na Hamisi Mcha ‘Vialli’ na Samir Hajji Nuhu wote wa Azam
FC.
Wengine
walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam FC), mabeki; Amir
Maftah (Simba), Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nasoro Masoud
‘Chollo’ (Simba) na Aggrey Morris wa Azam FC.
Viungo ni
Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngassa (Simba), Frank Domayo (Yanga), Amri
Kiemba (Simba), Athumani Idd ‘Chuji’ (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar),
wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), John
Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga).
Post a Comment