
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba
akizungumza na waandushi wa Habari, leo, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha na Bashir
Nkoromo
---
NA BASHIR
NKOROMO,
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, baada ya kuutumia mwaka 2012 kupanga safu ya uongozi katika chaguzi za ngazi zote zilizomalizika hivi karibuni, mwaka ujao wa 2013 utakuwa wa kuchapa zaidi.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, baada ya kuutumia mwaka 2012 kupanga safu ya uongozi katika chaguzi za ngazi zote zilizomalizika hivi karibuni, mwaka ujao wa 2013 utakuwa wa kuchapa zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Mwigulu Nchemba (pichani) alisema, kazi itakayofanywa na CCM katika mwaka huo,
ni pamoja na kukagua upya utekelezaji wa ilani ya CCM na kuhakikisha zile
ambazo hazikamilika zinamalizwa.
"Mwaka huu wa 2012 unaomalizika tuliutumia zaidi
kujipanga katika uchaguzi wa ngazi zote ili kupata safu nzuri itakayoisimamia
serikali kutekeleza ilani ya CCM, sasa mwaka mpya wa 2013 utakuwa wa kazi zaidi
za kusimamia serikali ili kuhakikisha mwaka 2015 mpiganaji wa CCM tutakayemteua
kugombea urais anapita kiulaini", alisema Mwigulu.
Akizungumzia tukio la Mbunge wa Arusha Godless Lema
kushinda rufani yake dhidi ya hukumu iliyomvua ubunge Aprili mwaka huu, Mwigulu
alisema, ushindi huo ni ushahidi kwamba serikali ya CCM inaongoza kwa misingi
ya utawala bora ambapo kila anayestahili haki anapata.
"Ushindi huu wa Lema, siyo kwamba anaakili sana
au chama chake kina maarifa sana yaliyosababisha ushindi, ila ni kutokana na
serikali ya CCM iliyopo madarakani kuheshimu na kujali haki na kwa kweli
natumia fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuthamini na kusimamia haki wakati
wote.. Ninyi si mnajua katika nchi zisizo na utawala bora jinsi ambavyo mambo
huwa kwenye kesi kama hizi. lakini hapa Tanzania ni tofauti kabisa", alisema,
Mwigulu.
Aliwashangaa Chadema akisema, "Hawa ni watu wa
aina yao, waliposhindwa katika kesi Arusha walisema Ikulu imeingilia na majaji
hawajui kiingereza.. sasa leo wameshinda wanafurahi na kuona kwamba sasa majaji
wanajua kiingereza na hawakuigusa Ikulu kwamba imeingilia, maana pale
ilipotolewa hukumu umbali wake ni hatua chache na Ofisi ya Ikulu kuliko
Arusha".
Mwigulu alitumia fursa hiyo kuwatakia heri
Watanzania kwa sikukuu za Krismas na mwaka mpya na kuwataka kuzitumia sikukuu
hizo kwa makini na kwa kiasi ili zisiwe chanzo cha matatizo kwao badala ya
furaha.
"Chama Cha Mapinduzi kinawatakieni sikukuu njema
za Krismas na mwaka mpya, lakini tunawaomba msherehekee kwa kiasi huku mkichunga
usalama wenu na mali zetu", alisema Mwigulu
Post a Comment