Kaimu mkuu wa mkoa wa
Singida, Manju Msambya (wa pili kushoto) akimkabidhi mwenyekiti wa kambi ya
kijiji cha Sukamahela wilayani Manyoni Bw. Nicolus Mkola Mkonongo, msaada
uliotolewa na rais Jakaya Kikwete kwa watu wenye ukoma kwa ajili ya X-Mass.Wa
kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi.Fatuma Toqufiki na wa pili kulia
ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fortunata
Malya.
Mwenyekiti wa kambi ya
kijiji cha Sukamahela wilayani Manyoni,Nicolus Mkola Mkonongo, ( wa kwanza
kushoto akitoa shukrani zake kwa mssada waliopewa na rasi Jakaya
Kikwete.
Baadhi ya msaada uliotolewa
na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kwa wakazi
wa kambi ya kijiji cha Sukamahela wilayani Manyoni,kwa ajili ya kufanikisha
sherehe ya X-Mass ya mwaka huu.Msaada huo uliokabidhiwa na kaimu mkuu wa mkoa wa
Singida,Manju Msambya ni pamoja na kilo 75 za mchele,lita kumi ya mafuta ya
kupikia vifurushi vidogo vya nyanya na vitunguu na beberu moja la
mbuzi
Post a Comment