Na : Heka Paul na Shakila Galus-
MAELEZO- Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa
chanjo duniani (GAVI) utakaonza kesho .
Mkutano huo unatarajiwa kuwa washiriki 600 kutoka
nchi mbalimbali duniani wakiwemo wake wa Marais , Mawaziri wa Afya, fedha na
watu mashuhuri kutoka nchi 73.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa jana(leo) mjini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu Regina Kikuli
inasema kuwa lengo la mkutano huo ni pamoja na kujadili mafanikio na changamoto
zinakabili huduma ya utoaji wa chanjo duniani.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa hii ni mara ya kwanza
mkutano wa aina hiyo kufanyika Afrika mashariki na kuongeza kuwa sababu
zilizopelekea mkutano kufanyika Tanzania ni pamoja na mafanikio makubwa katika
utoaji wa huduma za chanjo za watoto na mama
wajawazito.
Hivyo basi washiriki watapata fursa ya kutembelea
vituo vinavyotoa huduma za chanjo nchini ili kujionea mafanikio na changamoto
zilizopo pamoja na kujifunza.
Vilevile washiriki watapata fursa ya kujadili
masuala ya chanjo ikiwemo uingizwaji wa chanjo mpya na masuala ya afya ya mama
na mtoto.
Pia kutakuwepo na uzinduzi wa chanjo mbili mpya
za magonjwa ya kuhara, homa ya uti wa mgongio kwa watoto chini ya mwaka mmoja
ambazo zinatolewa nchini kwa hisani GAVI.


Post a Comment