 |
|
Wachezaji wa
Uganda wakimpongeza Geoffrey Kizito (anayetazama kamera amekumbatiana na Kiiza),
baada ya kufunga bao kwanza dakika ya nne dhidi ya Ethiopia katika Robo Fainali
ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye
Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala. Uganda ilishinda 2-0 bao lingine
likifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 60 na kwa ushindi huo, Uganda
itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao
utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na
Zanzibar.
chanzo: Bin Zubeiry
 |
|
Abdallah
Juma wa Kenya, akimdhibiti Rodrick Gonani wa Malawi katika Robo Fainali ya
kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge
Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini Kampala, Uganda. Kenya ilishinda 1-0, bao
pekee la Mike Barasa dakika ya 56 na sasa Harambee Stars itamenyana na Zanzibar
katika Nusu Fainali keshokutwa.
|
|
on Tuesday, December 4, 2012
Post a Comment