Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiangua kilio baada ya
kuwakumbuka wasanii wenzake Kanumba na Sharo.
Tukio hilo lilitokea kwenye
sherehe ya kutimiza miaka 13 ya Clouds FM, iliyofanyikia Club Bilicanas, Posta
jijini Dar es Salaa.
Kilio cha Shilole kilisababishwa na Mtangazaji wa Clouds
FM, Adam Mchomvu baada ya kutoa fursa ya kuwakumbuka wasanii maarufu
waliotangulia mbele ya haki.
...Shilole akiwa na simanzi baada ya kuwakumbuka
wasanii hao.
Akiwa jukwaani Mchomvu aliwaomba mashabiki waliojazana
ukumbini humo kunyanyua mikono juu na waliokuwa na simu aliwataka wazinyanyue
juu huku wakiwa wameziwasha ili zitoe mwanga.
Mtangazaji huyo alianza kuyataja
majina ya mastaa waliofariki mmoja baada ya mwingine, huku watu kibao wakionesha
simanzi zao.
on Thursday, December 6, 2012
Post a Comment