Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati
alipofungua rasmi Jengo la Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Kinyonga,wilayani
Kilwa jana wakati wa kilele cha ziara yake ya siku tano ya kikazi Mkoani
Lindi.Kulia aliyesimama ni Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dkt.Mike
Mabimbi.
Mganga mkuu
katika hospitali ya Kinyonga,wilayani Kilwa Dkt.Mike Mabimbi(kulia) akitoa
maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kufungua
jengo la wazazi katika hospitali hiyo na kulikagua.Wodi hiyo ya Wazazi imejengwa
ikiwa ni Mkakati wa kuboresha huduma ya Mama na mtoto Tanzania na ujenzi
umefadhiliwa na Halmashauri ya Kilwa pamoja na Chama Cha Madaktari Bingwa wa
Magonjwa ya akina mama Tanzania(AGOTA) na shirika la Uholanzi la Bioshape
Benefit Foundation.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria
mkutano wa hadhara mjni Kilwa Kivinje,mkoani Lindi jana
jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi mjni Kilwa Kivinje jana
jioni.Rais Kikwete aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi
amerejea jijini Dar es Salaam jioni hii.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akingalia wanafunzi wakifanya majaribio ya kisayansi
katika shule ya sekondari ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa, wakati alipokuwa
katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi jana.Picha na Freddy Mar
Post a Comment