Nyota wa Kilimanjaro Stars wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo Jijini Kampala leo. |
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakipasha mazoezini kwenye Uwanja wa Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo Jijini Kampala leo. |
Waleteni waleteni hao kina Okwi... Nyota wa Kili Stars wakijifua leo |
Tuko fitiii.... Kili Stars wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kyambogo Jijini Kampala leo. |
Erasto Nyoni (kulia) akitembea pembeni huku Mrisho Ngassa (katikati) akionyesha stamina zake za kubeba wachezaji wawili na Athuman Idd Chuji akishuhudia 'shughuli' |
KOCHA wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro
Stars, Kim Poulsen ameomba ‘fair play’ kutoka kwa muamuzi wa mechi ya kesho
dhidi ya The Cranes ya Uganda katika nusu fainali ya mashindano ya Cecafa
Challenge Cup Jijini Kampala.
Kocha huyo aliyasema hayo mara baada ya
Stars, inayodhamniniwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kumaliza mazoezi
katika Uwanja wa Chuo Kikuu Kyambogo.
“Vijana wamejiandaa vizuri kabisa na wote
wako katika hali nzuri ya kucheza ila tunachoomba ni fair play kutoka kwa
muamuzi maana tunacheza na wenyeji ambao wana watazamaji wengi,”
alisema.
Alisema timu zote mbili ni nzuri na iwapo
muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano mkali. “Vijana wana ari na
mchezo huu na tukipewa fair play tutacheza vizuri kama tulivyofanya katika
michezo dhidi ya Rwanda,” alisema Poulsen.
Muamuzi wa mechi ya Cranes na Stars ni
Mohamed El Fadil kutoka Sudan ambaye pia alichezesha mechi ya Stars dhidi ya
Rwanda.
Alisema ana furaha kwa kuwa hakuna majeruhi
hata mmoja na pia aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya
hali ya juu. “Hawa wanakaa kama familia si unawaona walivyo pamoja?” alisema
Poulsen na kuongeza kuwa hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.
Naye kocha msaidizi, Sylvester Mash alisema
Stars ina nafasi kubwa sana ya kushinda mechi hii kwa sababu wenyeji wao, The
Cranes watakuwa wanacheza kwa wasiwasi kwa kuwa wako nyumbani .
“Timu yetu iko motivated kabisa na
ukizingatia Uganda wako nyumbani, wao ndio wana tension kubwa zaidi,” alisema na
kuongeza kuwa mchezo huu utakuwa wa kusisimua sana.
Akizungumza kutoka Dar es Salaam, Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema Stars ina kila sababu
ya kutinga fainali na kunyanyua kombe kwa mara ya nne.
“Sisi kama wadhamini tunasubiri ushindi maana
tuna imani na Stars na hatua waliyofikia ni nzuri nay a kutia moyo kwa hivyo
watanzania wajitokeze kwa wingi na kuufuatilia mchezo huu kesho,” alisema
Kavishe.
Mchezo wa Stars na Cranes utatanguliwa na
semi fainali ya kwanza kati ya Zanzibar na Kenya ambao pia ni mchezo wa
kusisimua kwani timu zote mbili zimeshaonyesha uwezo mkubwa.
Kocha wa Zanzibar Salum Nassor ameshatangaza
mara mbili akiwa Zanzibar na hapa Kampala kuwa iwapo hataondoka na kombe basi
atabwaga manyanga.
Fainali na Cecafa Challenge zinatarajiwa
kufanyika Jumamosi Disemba 8 na mechi ya kumpata mshindi wa tatu na nne
itachezwa siku hiyo hiyo pia.
Post a Comment